Isura ye 3
1 Je, tutumbwile kuisifia bene kae? Tuhitaji kwaa barua ya mapendekezo kwinu au boka kwinu, kati baadhi ya bandu, je twahitaji? 2 Mwenga mwabene ni barua yitu ya mapendekezo, yaiandikilwe mu'mioyo yitu, yaiyowanika na kusomwa na bandu bote. 3 Na mwaonesha panga mwenga ni barua boka kwa Kristo, yaitolewa ni twenga, iandikilwe na wino kwaa ila kwa Roho wa Nnongo ywabile nkoto. Iandikilwe kwaa nnani ya vibao ya maliwe, ila nnani ya vibao vya mioyo ya bandu. 4 Na wolo nga ujasiri tubile nao katika Nnongo pitya Kristo. 5 Twajiamini kwaa wabene kwa kudai chochote kati boka kwitu. Badala yake, kujiamini kwitu kwaboka kwa Nnongo. 6 Ni Nnongo ywabile atupangite tuweze pangika atumishi wa liagano lyayambe. Ayee nga liagano labile kwaa lya barua ila ni lya Roho. Kwa kuwa barua ubulaga, lakini roho yatoa ukoto. 7 Nambeambe kazi ya kiwo itichongwa katika herufi nnani ya maliwe iisile kwa namna ya utukufu panga bandu ba Israeli balilinga kwaa bene ila pitya minyo ga Musa. Ayee nga sababu ya utukufu wa minyo gake, utukufu ambao wabile wafifia. 8 Je, kazi ya Roho ilowa kuwa kwaa na utukufu muno? 9 Kwa kuwa kati huduma ya hukumu ibile na utukufu, ni mara ilenga zaidi huduma ya haki huzidi muno katika utukufu! 10 Ni kweli panga, chelo chakipangilwe utukufu kwanza kibile kwaa utkufu kae katika heshima yee, kwa sababu ya utukufu wanansima. 11 Kwa kuwa kati chelo ambacho chabile chapeta chabile ni utukufu, ni kwa kiasi gani muno chelo ambacho ni chakudumu kibile na utukufu! 12 Kwa kuwa twajiamini eyo, tubile ni ujasiri muno. 13 Tubile kwaa kati Musa, ywabekite utaji nnani ya uso bake, ili panga bandu ba Israeli baweze kwaa lola moja kwa moja mu'mwisho wa utukufu ambao ubile watiboka. 14 Lakini malango gabe gatabilwe. Hata mpaka lisoba lee utaji wowolo bado ulekilwe nnani ya usomaji wa liagani lya kale. Ibekilwe kwaa wazi, kwa sababu ni katika Kristo kichake iondolewa kutalu. 15 Lakini hata leno, wakati wowote Musa asomwapo, utaji utama nnani ya mioyo yabe. 16 Lakini mundu paakeleka kwa Ngwana, utaji ulowa boka. 17 Nambeambe Ngwana ni Roho. Pabile ni Roho wa Ngwana, kubile ni uhuru. 18 Nambeambe twenga twabote, pamope ni minyo zibile kwaa bekewa utaji, ubona utukufu wa Ngwana. Twabadilishwa nkati ya muonekano wowolo wa utukufu boka shahada jimo ya utukufu yenda yenge, kati yaibile kwa Ngwana, ambaye ni Roho.